Wapandishwa mahakamani kwa tuhuma za kubaka na kulawiti Tanzania

 

Wapandishwa mahakamani kwa tuhuma za kubaka na kulawiti Tanzania

.

Watu wanne wanaotuhumiwa kumbaka na kumlawiti binti mmoja nchini Tanzania wamefikishwa mahakamani leo jumatatu na kusomewa mashtaka mawili.

Vyombo vya Habari nchini humo vimeripoti kuwa watuhumiwa hao wamefikishwa katika mahakama ya kanda Dodoma na kusomewa mashtaka mawili ikiwemo kubaka kwa kikundi na kumwingilia kinyume na maumbile binti mmoja.

Watuhumiwa hao wamekana mashtaka hayo kwa mujibu wa Mkurugenzi msaidizi wa ofisi ya mashtaka ya mahakama kuu.

Aidha kesi hiyo itaendelea kusikilizwa kwa siku tano mfululizo hadi ijumaa wiki hii.

Awali, Jeshi la polisi nchini Tanzania lilijitenga na kauli inayodaiwa kutolewa na aliyekuwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma dhidi ya binti huyo anayedaiwa kubakwa.

Kamanda huyo wa Polisi Theopista Mallya alinukuliwa akisema kuwa binti huyo alikuwa kama anajiuza, yaani kahaba. Licha ya kuikana kauli hiyo polisi pia waliwaomba radhi watu wote waliochukizwa na matamshi hayo.

Kutokana na hilo, Mkuu wa polisi nchini humo amemhamisha Kamanda Mallya kutoka kuongoza polisi Dodoma na kumrejesha makao makuu ya Polisi.

Comments

Popular posts from this blog

Hukumu aliyopewa mwanamume aliyembaka na kumuua muathiriwa yazua ghadhabu Ethiopia

Marekani inarudia makosa ya USSR katika Mashariki ya Kati

Putin anaweka wazi kuwa mazungumzo na Kiev sasa hayawezekani - Lavrov