Hukumu aliyopewa mwanamume aliyembaka na kumuua muathiriwa yazua ghadhabu Ethiopia

 

Hukumu aliyopewa mwanamume aliyembaka na kumuua muathiriwa yazua ghadhabu Ethiopia

.

CHANZO CHA PICHA,KWA HISANI YA FAMILIA

Tukio la ubakaji na mauaji ya kikatili kwa msichana wa miaka saba limesababisha hasira nchini Ethiopia, huku wengi wakisema hukumu iliyotolewa kwa mshambuliaji wake ni ndogo mno.

Heaven Awot alinajisiwa, kukatwa viungo na akauliwa na mwenye nyumba walikokuwa wakiishi Getnet Baye Agosti mwaka jana katika jiji la kaskazini-magharibi la Bahir Dar eneo la Amhara.

Getnet alihukumiwa kifungo cha miaka 25 jela. Kesi hiyo ilizua gumzo baada ya kukata rufaa hivi majuzi, na kesi hiyo sasa imeahirishwa hadi Oktoba.

Mamake msichana huyo, Abekyelesh Adeba, ameiambia BBC kwamba kumpoteza mtoto wake kumemfanya ajihisi "hafai kuwa hai".

Zaidi ya watu 200,000 kufikia sasa wametia saini ombi la mtandaoni la kutaka kuangaliwa upya kwa hukumu hiyo "kuonyesha uzito wa uhalifu" na kutoa msaada kwa mama anayeomboleza.

Comments

Popular posts from this blog

Marekani inarudia makosa ya USSR katika Mashariki ya Kati

Putin anaweka wazi kuwa mazungumzo na Kiev sasa hayawezekani - Lavrov