Vikosi vya Urusi vyadai kuuteka mji mwingine mashariki mwa Ukraine
Vikosi vya Urusi vyadai kuuteka mji mwingine mashariki mwa Ukraine

Jeshi la Urusi linasema kuwa limeuteka mji mdogo mashariki mwa Ukraine unaoitwa Niu-York, kama sehemu ya harakati zake kuelekea maeneo makubwa ya watu katika eneo la Donetsk.
Jeshi la Ukraine halijathibitisha kutekwa kwa mji waq Niu-York, likisema tu kwamba vikosi vya Urusi vinashambulia karibu na mji huo na maeneo mengine. Jeshi linafanya kashambulizi hayo "kwa makabiliano yanayostahili ... na mapigano yanaendelea", lilisema.
Ingawa ni makazi madogo tu, kuudhibiti mji wa Niu-York kunaweza kuonyesha hatua nyingine kuelekea maeneo ya kati yajimbo la Donetsk Toretsk na Pokrovsk.
Inadhaniwa kuwa moja ya malengo ya Ukraine kuteka eneo katika eneo la Kursk nchini Urusi ni kuilazimisha Urusi kuhamisha baadhi ya vikosi vyake mbali na eneo la mapigano la mashariki.
Hakuna dalili hadi sasa ya hilo kutokea, licha ya kamanda mkuu wa Ukraine Oleksandr Syrskyi kudai udhibiti wa vijiji na miji 93 ya Urusi.
Rais Volodymyr Zelensky alielezea hali ya vita vya mashariki kuwa ngumu, lakini akasema wanajeshi wa Ukraine wanafanya kila wawezalo kuangamiza vikosi vya Urusi.
Comments
Post a Comment