Usalama wa nyuklia unazorota Ukraine, yasema UN
Usalama wa nyuklia unazorota Ukraine, yasema UN

Hali ya usalama wa nyuklia katika kinu cha kuzalisha umeme cha Zaporizhzhia huko Ukraine inayokaliwa na Urusi inazidi kuzorota, mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kudhibiti nyuklia amesema, kufuatia shambulio la ndege zisizo na rubani karibu na eneo la eneo hilo.
Rafael Grossi, mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA), alisema bado "ana wasiwasi sana" na kutoa wito "kuwe na kizuizi cha juu kutoka pande zote" kulinda mtambo huo.
Shirika hilo lilisema athari za shambulio hilo zilikuwa kwenye barabara iliyo nje kidogo ya kituo hicho karibu na madimbwi muhimu ya kunyunyizia maji na takribani mita 100 kutoka kwenye njia pekee iliyobaki ya umeme wa juu.
Kiwanda hicho kilitekwa na vikosi vya Urusi katika vita hivyo na kimekuwa chini ya mashambulizi ya mara kwa mara ambayo pande zote mbili zimelaumiana.
Wiki iliyopita, Kyiv na Moscow zilitupina lawama baada ya moto kuzuka katika moja ya minara ya kupozea vinu hivyo.
IAEA haikusema ni nani aliyetekeleza shambulio hilo la Jumamosi, lakini timu yake iliyoko Zaporizhzhia ilisema uharibifu huo ulionekana kusababishwa na ndege isiyo na rubani iliyobeba kilipuzi.
"Timu imesikia milipuko ya mara kwa mara, bunduki nzito na milio ya risasi na mizinga katika umbali mbalimbali kutoka kwenye mtambo huo," shirika hilo lilisema katika taarifa.
Kiwanda hicho hakijazalisha umeme kwa zaidi ya miaka miwili na vinu vyote sita vimefungwa tangu Aprili.
Comments
Post a Comment