Ukraine yasema imeharibu daraja la pili la Urusi
Ukraine yasema imeharibu daraja la pili la Urusi

Ukraine inasema imeharibu daraja la pili la kimkakati katika kipindi cha wiki moja wakati ikiendelea na uvamizi wake katika eneo la Kursk nchini Urusi.
Jeshi la Ukraine siku ya Jumapili lilitoa picha za angani za shambulio hilo katika daraja hilo - linaloripotiwa kuwa juu ya mto Seym mjini Zvannoe.
Saa chache baadaye, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alisema malengo ya uvamizi wa kijeshi katika Kursk ni pamoja na kuundwa kwa "eneo la lisilo na mapigano" ili kuzuia mashambulizi ya Urusi.
Inakaribia kufikia wiki mbili tangu Ukraine ianzeshambulio lake kubwa zaidi katika ardhi ya Urusi tangu Moscow ilipoanzisha uvamizi wake wa Ukraine mnamo 2022.
"Minus daraja moja zaidi," kamanda wa jeshi la anga la Ukraine Luteni Jenerali Mykola Oleschuk aliandika kwenye mitandao ya kijamii akiwa na picha za shambulio hilo.
Jenerali Oleschuk aliongeza kuwa: "Kikosi cha anga cha Ukraine kinaendelea kumnyima adui uwezo wa vifaa na mashambulizi ya anga ya usahihi, ambayo kwa kiasi kikubwa yamezuia malengo ya adui."
Video hiyo inaonyesha wingu kubwa la moshi juu ya daraja na moja ya sehemu zake inaonekana kuharibiwa. Haijulikani ni lini shambulio hilo lilifanyika.
Comments
Post a Comment