Ukraine yaamuru kuhamishwa kwa wakazi wa mji huku Urusi ikipata mafanikio

 

Ukraine yaamuru kuhamishwa kwa wakazi wa mji huku Urusi ikipata mafanikio

f

CHANZO CHA PICHA,REUTERS

Mamlaka ya Ukraine imeamuru kuhamishwa kwa watu kutoka mji muhimu katika eneo la Donbas huku vikosi vya Urusi vikiendelea kupata mafanikio mashariki mwa nchi hiyo, licha ya mashambulizi yanayoendelea ya Ukraine katika eneo la Kursk nchini Urusi.

Maafisa walisema familia zilizo na watoto wanaoishi Pokrovsk na vijiji vya jirani watalazimika kuondoka.

Mkuu wa serikali ya kijeshi ya mji huo, Serhii Dobriak, amesema wakazi walikuwa na angalau na wiki mbili kukimbia kabla ya kusonga mbele kwa Urusi.

Mji huo muhimu kimkakati ni moja wapo ya ngome kuu za ulinzi za Ukraine na kitovu muhimu cha vifaa kwa wanajeshi wa Ukraine upande wa mashariki.

Comments

Popular posts from this blog

Hukumu aliyopewa mwanamume aliyembaka na kumuua muathiriwa yazua ghadhabu Ethiopia

Marekani inarudia makosa ya USSR katika Mashariki ya Kati

Putin anaweka wazi kuwa mazungumzo na Kiev sasa hayawezekani - Lavrov