TEC: Kutowasikiliza Wamasai wa Hifadhi ya Ngorongoro ni kuwanyima haki zao
TEC: Kutowasikiliza Wamasai wa Hifadhi ya Ngorongoro ni kuwanyima haki zao

Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC) wamesema kutowasikiliza Wamaasai wanaioshi katika eneo la Hifadhi ya Ngorongoro ni kuwanyima haki zao.
Kauli hiyo inakuja wakati mamia ya vijana na wakina mama wa eneo hilo walipoandamana jana wakiishinikiza Serikali kuwapa huduma za mbalimbali za kijamii.
Akizungumza jana, Katibu wa TEC Padri Charles Kitima alisema, "Leo hii tunapozungumza ndugu zetu Wamasai wa kule Ngorongor wanatuma ujumbe mbaya wenye twasira hasi Kimataifa… “…unapowaeleza ni hiari yao kubaki Ngorongoro halafu ukiwanyima haki zao za msingi huo ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu, alisema Kitima.
Siku ya jana inaelezwa kuwa maandamano ya amani yaliyofanywa na jamii ya wamasaai yalidumu kwa takribani saa nen huku shughuli za utalii zikilazimika kusimama.
Watetezi wa haki za binadamu nchini Tanzania pia wamezitaka mamlaka za Tanzania kuheshimu haki za jamii hiyo kwa kusikiliza na kuwapa mahitaji yao ya msingi.
Tangu mwaka 2022, Mamlaka nchini Tanzania zimekuwa zikiendesha zoezi la kuhamisha watu kutoka eneo hilo la hifadhi kwenda kwenye eneo la Msomera mkoani Tanga.
Hata hivyo, tangu kuanza kwa zoezi hilo takribani watu 7,000 wameshahama kwa hiari huku baadhi wakieleza kutokuwa tayari kuhama.
Comments
Post a Comment