Tanzania: Polisi waomba radhi kwa kauli kuhusu binti anayedaiwa kubakwa

 

Tanzania: Polisi waomba radhi kwa kauli kuhusu binti anayedaiwa kubakwa

Jeshi la polisi nchini Tanzania limejitenga na kauli inayodaiwa kutolewa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma dhidi ya binti anayedaiwa kubakwa katika taarifa iliyochapishwa na Gazeti la Mwananchi.

Katika taarifa Jeshi la polisi limeelezea kuchukizwa na taarifa hiyo inayosambaa kwenye vyombo vya habari wakati ufuatiliaji ukifanyika kupata usahihi wake.

Gazeti hilo limemnukuu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma akiashiria katika mahojiano na mwandishi wake kwamba mwanamke aliyebakwa na kulawitiwa alikuwa ‘’anajiuza.’’

Jeshi la polisi pia limesisitiza kwamba huo sio msimamo wake.

‘’Kauli sahihi ni kama zilivyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi kwa umma Agosti 4, 6 na 9, 2024,’’ ilisema katika taarifa na kuongeza kuwa watuhumiwa watafikishwa mahakamani Agosti 19.

Comments

Popular posts from this blog

Hukumu aliyopewa mwanamume aliyembaka na kumuua muathiriwa yazua ghadhabu Ethiopia

Marekani inarudia makosa ya USSR katika Mashariki ya Kati

Putin anaweka wazi kuwa mazungumzo na Kiev sasa hayawezekani - Lavrov