Safari za ndege zafutwa baada ya mkasi kupotea Japan
Safari za ndege zafutwa baada ya mkasi kupotea Japan

Safari 36 za ndege zilikatishwa na 201 kucheleweshwa katika uwanja wa ndege wa Japani mwishoni mwa juma baada ya mkasi kupotea katika eneo karibu na lango la kuabiri.
Ukaguzi wa usalama katika kituo cha ndani cha uwanja wa ndege wa New Chitose cha Hokkaido ulisitishwa kwa takriban saa mbili Jumamosi asubuhi, na kuwaacha mamia ya wasafiri wakiwa wamekwama kwa muda.
Kulikuwa na vizuizi vikubwa na foleni huku abiria waliokuwa kwenye chumba cha kuondoka wakilazimika kukagua usalama.
Wenye mamlaka walijaribu kutafuta mkasi uliokosekana, ambao ulipatikana katika duka moja siku iliyofuata.
Comments
Post a Comment