Mmoja afariki na Waingireza wengine hawajulikani walipo baada ya boti ya kifahari kuzama Italia

 

Mmoja afariki na Waingireza wengine hawajulikani walipo baada ya boti ya kifahari kuzama Italia

.

CHANZO CHA PICHA,FABIO LA BIANCA

Mtu mmoja amefariki na wengine sita hawajulikani walipo baada ya boti waliyokuwa wakisafiria kuzama katika ufuo wa Sicily mapema Jumatatu asubuhi, shirika la zimamoto na uokoaji la Italia limesema.

Boti hiyo yenye urefu wa mita 56 (futi 183) ilikuwa ikipeperusha bendera ya Uingereza na Waingereza ni miongoni mwa wasiojulikana walipo, vyombo vya habari vya Italia vimeripoti.

Watu 22 waliokuwemo ndani ni pamoja na wafanyakazi 10 na abiria 12, baadhi yao wakiwa raia wa Marekani na Canada. Huduma za dharura ziliokoa watu 15 akiwemo mtoto wa mwaka mmoja.

Vyombo vya habari vya eneo hilo viliripoti kwamba boti hiyo ilizama baada ya kukutana na dhoruba kali usiku kucha ambayo ilisababisha milio ya maji kujitokeza juu ya bahari.

Comments

Popular posts from this blog

Hukumu aliyopewa mwanamume aliyembaka na kumuua muathiriwa yazua ghadhabu Ethiopia

Marekani inarudia makosa ya USSR katika Mashariki ya Kati

Putin anaweka wazi kuwa mazungumzo na Kiev sasa hayawezekani - Lavrov