Miili sita ya mateka imeopolewa, jeshi la Israel linasema

 

Miili sita ya mateka imeopolewa, jeshi la Israel linasema

h

Miili ya mateka sita imeopolewa kutoka Ukanda wa Gaza, jeshi la Israel linasema.

Taarifa kutoka kwa Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) inasema miili ya Yagev Buchshtab, Alexander Dancyg, Avraham Munder, Yoram Metzger, Nadav Popplewell na Haim Perry iliopolewa kutoka eneo la Khan Younis siku ya Jumatatu.

Shughuli ya uopoaji ilifanywa na IDF pamoja na Shirika la Usalama la Israeli.

Jukwaa la familia za mateka lilisema kupatikana kwa miili hiyo kumezipa familia "kufungwa kwa lazima".

Taarifa hiyo iliendelea kusema kuwa kurejea kwa mateka 109 waliosalia kutoka Gaza "kunaweza tu kufikiwa kupitia makubaliano ya mazungumzo" na kuitaka serikali ya Israel "kufanya kila iwezalo ili kukamilisha mpango uliopo mezani kwa sasa".

Mazungumzo kuhusu makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyotafutwa kwa muda mrefu na kuachiliwa kwa mateka yanaendelea, huku waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken kwa sasa akiwa yuko Mashariki ya Kati akishinikiza kufikiwa makubaliano.

Siku ya Jumatatu, Bw Blinken alisema Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alikubali pendekezo la Marekani la makubaliano, baada ya wawili hao kukutana Tel Aviv.

Israel ilianzisha mashambulizi ya jeshi lake huko Gaza kujibu shambulio ambalo halijawahi kushuhudiwa kusini mwa Israel tarehe 7 Oktoba lililofanywa na wanamgambo wa Hamas, ambapo takriban watu 1,200 waliuawa na 251 kuchukuliwa mateka.

Zaidi ya watu 40,000 wameuawa Gaza tangu wakati huo, kulingana na wizara ya afya ya eneo hilo inayosimamiwa na Hamas.

Comments

Popular posts from this blog

Hukumu aliyopewa mwanamume aliyembaka na kumuua muathiriwa yazua ghadhabu Ethiopia

Marekani inarudia makosa ya USSR katika Mashariki ya Kati

Putin anaweka wazi kuwa mazungumzo na Kiev sasa hayawezekani - Lavrov