Miili 5 ilipatikana ndani ya boti ya kifahari iliyozama nchini Italia

 

  1. Miili 5 ilipatikana ndani ya boti ya kifahari iliyozama nchini Italia

    f

    CHANZO CHA PICHA,EPA

    Maelezo ya picha,Yacht ya kifahari ya Bayesian

    Wafanyakazi wa uokoaji wamepata miili 5 Jumatano ndani ya boti ya kifahari ya Bayesian, ambayo ilizama Jumatatu kwenye pwani ya Sicily, kusini mwa Italia.

    Boti hiyo ya kifahari yenye urefu wa mita 56 iliyokuwa ikipeperusha bendera ya Uingereza ilikuwa imebeba watu 22 (abiria 12 na wafanyakazi 10), akiwemo bilionea wa Uingereza na mtendaji mkuu wa benki ya Morgan Stanley.

    Boti hiyo, Bayesian ilizama katika dhoruba kali mapema Jumatatu asubuhi.

    Watu 15 waliokuwa ndani yake waliokolewa wakiwa hai na mtu mmoja akapatikana amekufa: mpishi wa boti, Recaldo Thomas.

    Bado mwili mmoja wa mwisho haujapatikana kati ya jumla ya sita waliopotea katika ajali hiyo.

    Watu ambao bado hawajapatikana wametajwa kuwa ni: tajiri wa teknolojia wa Uingereza Mike Lynch na binti yake mwenye umri wa miaka 18 Hannah; Mwenyekiti wa Kimataifa wa kampuni ya Morgan Stanley Jonathan Bloomer na mkewe Judy Bloomer; Chris Morvillo, wakili wa Marekani wa Lynch, na mkewe Neda Morvillo.


Comments

Popular posts from this blog

Hukumu aliyopewa mwanamume aliyembaka na kumuua muathiriwa yazua ghadhabu Ethiopia

Marekani inarudia makosa ya USSR katika Mashariki ya Kati

Putin anaweka wazi kuwa mazungumzo na Kiev sasa hayawezekani - Lavrov