Kenya: Maafisa wa jiji la Nairobi wawakamata watu kwa kujisaidia katikati ya jiji

 

Kenya: Maafisa wa jiji la Nairobi wawakamata watu kwa kujisaidia katikati ya jiji

g

CHANZO CHA PICHA,PUBLICIS PIXELPARK

Wakaazi 30 wa Nairobi wameripotiwa kukamatwa kwa kujisaidia haja ndogona kutupa uchafu katika Wilaya yenye shughuli nyingi kibiashara jijini Nairobi (CBD) kama sehemu ya hatua ya serikali ya kaunti ya Nairobi ya kukabiliana na makosa madogo.

Wakiongozwa na afisa mkuu wa Mazingira wa Nairobi Geoffrey Mosiria, timu za watekelezaji sheria za kaunti hiyo zwalishika doria katika mitaa iliyochaguliwa ya CBD ili kuwakamata Wakenya waliokiuka sheria hiyo.

Sheria ya Kero ya Umma ya Nairobi 2021 inasema kwamba mtu yeyote atakayepatikana akijisaidia haja ndogo au haja kubwa katika eneo la umma atawajibika kulipa faini ya Ksh.10,000, kifungo cha miezi sita jela au kupewa adhabu zote mbili.

Zaidi ya hayo, viongozi wa kaunti hiyo waliwaamuru wafanyabiashara wa barabarani kusafisha lundo lao la takataka na kuzitupa ipasavyo.

Wahalifu 30 walikamatwa Jumatatu usiku na kufikishwa katika mahakama ya jiji siku ya Jumanne ambayo iliwapatia adhabu ya kufanya kazi kwa manufaa ya umma katika vituo vya umma.

Miongoni mwa kazi hizo ni pamoja na kusafisha chumba cha kuhifadhia maiti cha jiji na uwanja wa Uhuru Park.

Comments

Popular posts from this blog

Hukumu aliyopewa mwanamume aliyembaka na kumuua muathiriwa yazua ghadhabu Ethiopia

Marekani inarudia makosa ya USSR katika Mashariki ya Kati

Putin anaweka wazi kuwa mazungumzo na Kiev sasa hayawezekani - Lavrov