Israel na Gaza: Je, kwanini mpango wa kusitsha mapigano wa Marekani ni mgumu kutekeleza?

 

Israel na Gaza: Je, kwanini mpango wa kusitsha mapigano wa Marekani ni mgumu kutekeleza?

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Anthony Blinken na waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu wakutana mjini Jerusalem.

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Anthony Blinken amesema usitishaji vita kati ya Israel na Hamas huko Gaza unaweza kufikiwa ndani ya siku chache baada ya Israel kukubali mpango wake wa amani tarehe 19 Agosti.

Makubaliano hayo yatahusisha kukomesha uhasama katika Ukanda wa Gaza na kurejea kwa mateka waliotekwa na Hamas na makundi mengine yenye silaha wakati wa shambulio la Oktoba 2023 dhidi ya Israel.

Marekani imekuwa ikijaribu kuandaa "mpango wa maelewano" ili kuondoa vikwazo katika makubaliano kati ya Israel na Hamas.

Je, ni mambo gani makuu ya mpango wa amani wa Marekani?

Blinken anasukuma mpango wa amani nchini Israel, kulingana na mpango ulioainishwa na Rais wa Marekani Joe Biden mwezi Mei.

Mpango huo utatekelezwa kwa awamu tatu.

Awamu ya kwanza ni pamoja na "kusitishwa kwa mapigano kwa jumla " kwa wiki sita, kuondolewa kwa wanajeshi wa Israekal tika maeneo yote ya makazi huko Gaza, na kubadilishana baadhi ya mateka, ikiwa ni pamoja na wanawake, wazee na waliojeruhiwa na wagonjwa, kwa wafungwa wa Kipalestina wanaozuiliwa kwenye jela za Israel.

Awamu ya pili itajumuisha kuachiliwa kwa mateka wengine wote waliosalia na "mwisho kukoma kwa uhasama."

Kufikia Novemba 2023, mateka 105 walirudishwa Israeli, na zaidi ya 100 walibaki Gaza.

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Israel inasema zaidi ya mateka 100 wamesalia, ambapo 71 wanaaminika kuwa hai. Mateka wengine wanne walikuwa Gaza kabla ya shambulio la Oktoba 7, wawili kati yao wanaaminika kuuawa.

Chini ya makubaliano yaliyofikiwa Novemba 2023, Hamas iliwaachilia mateka 105 wakati wa usitishaji mapigano wa wiki moja ili kubadilishana wafungwa wapatao 240 wa Kipalestina katika jela za Israel.

Makubaliano hayo ya amani yatajumuisha mpango wa kuijenga upya Gaza.

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Awamu ya tatu ya makubaliano hayo ya amani itajumuisha mpango mkubwa wa ujenzi mpya wa Gaza na kurejeshwa kwa mabaki ya mateka waliokufa.

"Waziri Mkuu alisisitiza ahadi ya Israel kwa pendekezo la sasa la Marekani la kuachiliwa kwa mateka, ambalo linazingatia mahitaji ya usalama ya Israeli na ambayo Waziri Mkuu anazingatia kwa dhati," serikali ya Israel ilisema katika taarifa yake mnamo Agosti 19.

Je, kuna ugumu gani katika mpango wa amani?

Tofauti kubwa bado inaonekana kati ya Israel na Hamas. Moja ya masuala ni kuendelea kuwepo kijeshi kwa Israel huko Gaza.

Israel imesema inataka wanajeshi wake kubaki mahali pake ili kuzuia Hamas kujipanga upya na kusafirisha silaha zaidi za magendo.

Hata hivyo, Hamas inapinga wanajeshi wa Israel kubaki Gaza baada ya kusitishwa kwa mapigano.

Hamas na Israel pia hazikubaliani kuhusu idadi na utambulisho wa wafungwa wa Kipalestina watakaorejeshwa Gaza badala ya mateka wa Israel.

Hamas haitaki wanajeshi wa Israel kukalia Gaza baada ya kusitishwa kwa mapigano.

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Kuna uwezekano gani wa makubaliano ya amani?

Blinken alisema makubaliano ya kusitisha mapigano lazima yafikiwe haraka.

"Huu ni wakati wa maamuzi, labda bora zaidi, labda nafasi ya mwisho ya kuwarudisha mateka nyumbani, kufikia usitishaji mapigano na kuweka kila mtu kwenye njia bora zaidi ya amani na usalama wa kudumu," Blinken alisema huko Israeli mnamo Agosti 19.

Waisraeli wengi wanashinikiza makubaliano ya amani na kurejeshwa kwa mateka wote waliosalia.

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Hata hivyo, Hamas ilisema haitatuma wawakilishi nchini Misri na Qatar.

"Tulifikia makubaliano (kupitia wapatanishi) mnamo Julai 2 ... kwa hivyo hatuhitaji duru mpya ya mazungumzo au kujadili madai mapya kutoka kwa Benjamin Netanyahu," alisema Basem Naim, mjumbe wa ofisi ya kisiasa ya Hamas iliyoko Qatar. .

Alisema Hamas imesalia na "nia" katika makubaliano ya amani, lakini akasema: "Tumeonesha kubadilika kwa kiwango cha juu na chanya, na upande mwingine ulitafsiri hii kama udhaifu na ulijibu kwa nguvu kubwa, hana nia ya kufikia usitishaji wa mapigano, lakini tu. anataka kuongeza mafuta kwenye moto katika ukanda ... na kutumikia maslahi yake binafsi ya kisiasa."

Serikali ya Israel ilijibu kwa kusema Hamas "haijabadilika kabisa" na kusema shinikizo zinahitajika kuwekwa kwa kundi hilo.

Wanajeshi wa Israel wanaendelea kuchimba na kuharibu vichuguu vya Hamas.

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Mnamo Oktoba 7, 2023, Hamas ilianzisha shambulio kusini mwa Israel, na kuua watu wapatao 1,200 na kuchukua mateka 251. Kisha jeshi la Israel lilianzisha operesheni ya kuwaangamiza Hamas huko Gaza.

Tangu wakati huo, zaidi ya watu 40,130 wameuawa huko Gaza, kulingana na Wizara ya Afya ya Gaza inayoendeshwa na Hamas.

Mapigano yanaendelea hadi leo. Israel inasema katika siku chache zilizopita imeharibu maeneo kadhaa ya Hamas na mtandao wa vichuguu, ambapo roketi na makombora yalipatikana, na kwamba jeshi lake "limeangamiza makumi ya magaidi."

Watu sita waliuawa katika shambulizi la anga la Israel huko Khan Yunis kusini mwa Gaza siku ya Jumatatu, huku wengine wanne wakiuawa katika shambulio lililolenga gari katika mji wa Gaza kaskazini mwa Gaza, vyombo vya habari vya Palestina viliripoti.

Ingawa Blinken alisema anaamini makubaliano ya amani yanaweza kufikiwa haraka, vyanzo vya Israel na Hamas vilivyohojiwa na BBC havikuwa na matumaini.

Comments

Popular posts from this blog

Hukumu aliyopewa mwanamume aliyembaka na kumuua muathiriwa yazua ghadhabu Ethiopia

Marekani inarudia makosa ya USSR katika Mashariki ya Kati

Putin anaweka wazi kuwa mazungumzo na Kiev sasa hayawezekani - Lavrov