Iran: Mahujaji 28 wa Pakistan wafariki katika ajali ya basi
Iran: Mahujaji 28 wa Pakistan wafariki katika ajali ya basi

Basi lililokuwa limebeba mahujaji wa Pakistani limepinduka nchini Iran na kuua takriban abiria 28, vyombo vya habari vya serikali ya Iran vimeripoti.
Ajali hiyo ilitokea Jumanne usiku katika jimbo la kati la Iran la Yazd na ilitokana na hitilafu ya breki, Reuters imesema, ikinukuu uchunguzi wa awali wa polisi.
Abiria wengine 23 walijeruhiwa, 14 kati yao wakiwa mahututi, balozi wa Pakistani nchini Iran Muhammad Mudassir Tipu aliambia BBC.
Mahujaji hao walikuwa wakisafiri kutoka mkoa wa Sindh nchini Pakistan kuelekea mji mtakatifu wa Karbala nchini Iraq ili kuadhimisha moja ya matukio makubwa katika kalenda ya Shia.
Takriban watu 50 wanaaminika walikuwa kwenye basi hilo wakati wa ajali hiyo, kulingana na vyombo vya habari vya ndani, wakiwemo mahujaji kutoka Larkana, Ghotki na miji ya Sindh.
Wanawake 11 na wanaume 17 ni miongoni mwa waliofariki katika ajali hiyo, kulingana na mkurugenzi wa usimamizi wa mgogoro Ali Malekzadeh.
Basi hilo lilishika moto mbele ya kituo cha ukaguzi cha Dehshir-Taft nchini Iran, karibu kilomita 681 (maili 423) kusini mwa mji mkuu Tehran, kulingana na ripoti za vyombo vya habari vya ndani.
Comments
Post a Comment