DRC: Takriban watu 24 wafa maji baada ya boti yao kupinduka

 

DRC: Takriban watu 24 wafa maji baada ya boti yao kupinduka

d

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,Boti zinazobeba abiria kwenye Mito ya Kongo mara nyingi hazitunzwa vizuri na zinajaa kupindukia

Takriban watu 24 wamefariki katika Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo baada ya mashua iliyokuwa imejaza mizigo kupinduka kwenye mto katika jimbo la Mai-Ndombe nchini Kongo, na idadi ya vifo inatarajiwa kuongezeka huku abiria wengi wakitoweka, afisa mmoja wa eneo hilo alisema Jumatano.

Boti iliyobeba takriban abiria 250 hadi 300 ilipinduka Jumapili usiku baada ya kugonga vizingiti chini ya maji, msimamizi wa eneo la Kutu Jacques Nzenza aliliambia shirika la habarila Reuters.

Kupakia watu na miziko kupita kiasi ndio chanzo kikuu cha ajali hiyo, alisema. "Kulikuwa na wasi wasi katika boti na watu waliojawa na hofu walienda kwenye sehemu moja kuweka uzito upande mmoja, na kusababisha mashua kupinduka."

Kiongozi wa jumuiya ya kiraia katika eneo hilo, Fidele Lizoringo, amesema watu 43 walinusurika lakini wanakijiji waliokuwa na hasira walimpiga meneja wa boti hiyo kwa sababu baadhi ya ndugu zao walikufa katika ajali hiyo.

Usafiri wa kwenye mito na ajali mbaya za boti ni jambo la kawaida katika nchi hiyo ya Afrika ya kati, ambayo ina barabara chache za lami katika eneo lake kubwa lenye misitu na vyombo vya usafiri mara nyingi hupakiwa kupita uwezo wake.

Comments

Popular posts from this blog

Hukumu aliyopewa mwanamume aliyembaka na kumuua muathiriwa yazua ghadhabu Ethiopia

Marekani inarudia makosa ya USSR katika Mashariki ya Kati

Putin anaweka wazi kuwa mazungumzo na Kiev sasa hayawezekani - Lavrov